Bongo Bomba! Poem by Meshack Sewe

Bongo Bomba!



Niongeapo na waTanga,

Wengi hucheka wakitanga,

Lugha sanifu wamepanga,

Sauti yao ncha ya panga,

Hawana rabsha ya 'makanga',

Watakukaribisha boda Namanga.

Utani kweli wao 'humanga'

Wadada wajua hufunga kanga!

Fika Bongo upate visanga!

Ustaarabu hata kwa wachanga

Udugu kwao ni kama nanga

Wasanii kibao hata wa uganga!

Kufunga macho mjini janga!

Usishaangae huna shanga!


2008©Meshack Sewe

(My first attempt at writing a poem('shairi) in Swahili language)

COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success