SPASIBA
Spasiba,
spasiba.
Kwa mwenyezi,
bila kipimo nakuenzi.
Spasiba,
spasiba.
Kwa mama ulileta duniani,
na kunilea.
Spasiba,
spasiba.
Kwa marafiki wa kikweli,
sio wahuni.
Spasiba,
spasiba.
Kwa wahusika wote wenye nia njema,
sio wenye sumu kwenye sindano.
Spasiba,
spasiba.
Kwa maadui washirikina na wenye fitina,
wasio na utu ila tu unafiki.
Garagazano hili,
hamwezi.
Spasiba,
spasiba.
LiterarySpaceAfricaIan Munywe©
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem