Tumbuizo Langu Poem by ckim mbasa

Tumbuizo Langu

Rating: 5.0

We ni tumbuizo la macho ukitembea,
Kwa maringo watazamwa ukisogea,
Malkia mtanashati wa mwili uliolegea,
Mitaani mwendowo ni kigezo cha kutegemea,
Mwili laini maji yakunde kuogea,
Si yangu ila maoni nangojea,

Tutembeapo pamoja kufikiria, mikono tumeshikana
Kama ndege wawili wapenzi wakaapo pamoja
Usiku wa baridi wenye pepo kali
Kukaa sako kwa bako huku tumeandika nne
Tukijiviringisha kiawanjani kama kunguru awindapo panzi
Tukichekeleana na kubusu kama punguani

Kuamka nawe ni tumbuizo ya macho ukitembea
Fikiria tutembeapo hivi kama mtu mmoja
Kama mzigo ni ufunguo wa kila kitu
Sote twaitumia mizigo yetu kuwasilisha ujumbe
Mikono na nyoyo zetu zikibanana mwanzoni
Nafikiri yote ni hivyo kwasababu ni yeye.

COMMENTS OF THE POEM
Vishal Sharma 11 June 2013

nice poem enjoyed your words

1 0 Reply
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success