Raha Ya Choo Poem by Abdallah Mpogole

Raha Ya Choo

Rating: 3.5

Salaam zenu Malenga, karibuni chooni kwangu.
Nimeshindwa kujivunga, kwani haja Dondandugu.
Choo changu nakipanga, kinitibu haja zangu.
Raha ya choo najua, Na sio cha kudowea.

Choo changu ki karibu, hatua chache najongea.
Si choo cha nasibu, tunu ya wapitanjia,
Si choo cha kuwa Bubu, kwa harufu kunukia.
Raha ya choo mvuto, kiingia taki toka.

Choo changu ki liwazo, nasonona ugenini.
Nikutapo vya uozo, najutia ni kwanini.
Nalipia kwa viwango, hudumaze si yakini.
Raha ya choo hisia, mfano wa kwamini dini.

Choo hiki maridhia, sikosi kuhudhuria.
Hakiye kugugumia, kwa nidhamu naachia.
Mtu chake kusifia, si choo cha Abiria.
Raha ya choo kufungwa, funguoze kibindoni.

Kwa dharura natumia, kile cha kuchuchumaa.
Cha kukaa maramia, siku zote chanifaa.
Tenkile lilotimia, maji yamwagika pwaa.
Raha ya choo usafi, kibanwa husiti kwenda.

Epa choo ujamaa, hujakaa kimegongwa.
Ati nguo ukivaa, kwa harufu inazongwa.
Choo Nzi wametwaa, ka nyuki kwenye mzinga.
Raha ya choo kukonga, pigwapo simu walonga.

COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Abdallah Mpogole

Abdallah Mpogole

Iringa, Tanzania
Close
Error Success