Binti Mtu Poem by ckim mbasa

Binti Mtu

Kwako naja shangazi,
Sija panda ngazi,
Kwani mi si mkwezi,
Eti ‘mekuletea nazi,
Binti mtu ka tamka wazi,
Kajibu mlango wazi,
Kakaribishwa wazi wazi,
Wakila sinia za viazi,
Kajazwa bashasha kuwa ‘mepata msaidizi,

Mtulivu- vu
Pia mnyenyekevu

Sikujua
Jiji litamzuzua
Haaaaaaaaaaa,

Siku moja katokwa za kwetu
Kumkuta kavaa kama super star,
Mtaani kujulikana kuzidi mayor,
Vilabuni hakosi,
Anataka simu mbili,
Chakula cha kiafrika hali tena
Kastaarabika kuzidi kiwango.

Mguu huu ni wako, waona kavinjari
Mpe mpe mpe maji ya jokofu anywe,
Kwami nyumbani jokofu ni mtungi
Ya mtungini kadada hapendi tena
Nunua blackberry, a surf usiku kucha
Swimming pool mletee uwanjani,
Kwamazoea yake sasa aogelee
TV mletee,
Na spaghetti mpikie
Alale unono kwa matanda ya kimalkia,

Nasema uuuuuuuuuuuuuu u u

COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success